Kishida ataka kukukatana na Kim Jong Un wa Korea kaskazini
25 Machi 2024Matangazo
Vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini vimeripoti taarifa hiyo.
Waziri Mkuu wa Japan Kishida amesema anataka kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini bila ya masharti yoyote na anasimamia juhudi za kufanikisha lengo la kufanyika mkutano huo wa kwanza tangu miaka 20 iliyopita.
Hata hivyo Kim Jong Un amejibu kwa kusema kuboreshwa uhusiano kati ya Japan na Korea Kaskazini kutategemea iwapo Japan itafanya maamuzi ya kisiasa yanayokubalika. Japan iliitawala rasi yote ya Korea kuanzia mwaka 1910 hadi mwaka 1945.