1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Blinken yuko Ufaransa kuijadili Mashariki ya Kati

8 Januari 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayemaliza muda wake Antony Blinken ameanza ziara yake mjini Paris, Ufaransa leo Jumatano.

https://p.dw.com/p/4oxLK
 Antony Blinken
Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani Antony BlinkenPicha: Andrew Caballero-Reynolds/AP Photo/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayemaliza muda wake Antony Blinken ameanza ziara yake mjini Paris, Ufaransa leo Jumatano ambapo atapokea heshima ya juu kabisa ya Ufaransa na kutafuta ushirikiano zaidi kuhusu eneo lenye  misukosuko la Mashariki ya Kati.

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani aliwasili mapema Jumatano mjini Paris akitokea Japan na Korea Kusini. Safari hii inatarajiwa kuwa ya mwisho kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Marco Rubio mara baada ya Rais mteule Donald Trump kuapishwa Januari 20. Hayo ni kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa shirika la AFP aliyeongozana nae katika safari hiyo.

Blinken atakutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye atamkabidhi nishani ya heshima ya juu zaidi ya Ufaransa. Blinken mwenyewe ambaye alitumia sehemu ya utoto wake katika viunga vya Paris amezungumzia jukumu la Ufaransa katika kuunda mtazamo wake wa ulimwengu.

Blinken pia atakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot kwa mazungumzo yanayoangazia Mashariki ya Kati ikiwa ni pamoja na Syria.