1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wazanzibari kupokea chanjo ya Covid-19 kabla Hija?

17 Mei 2021

Rais wa Zanzibar Dokta Hussein Mwinyi, aliwataka waumini wa Kiislamu wenye nia ya kufanya Ibada ya Hijja kujitayarisha wakati ambapo Saudi Arabia imetangaza kutowaruhusu wasiochomwa chanjo ya virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3tVPg
Saudi-Arabien Mekka | Erste Pilger nach Coronasperrung
Picha: Saudi Ministry of Hajj and Umra/AFP/Getty Images

Kauli yake hii katika Baraza la Iddi wiki iliyopita imetafsiriwa na wengi kwamba hatimaye Zanzibar nayo inataka kufuata itifaki ya kilimwengu katika kukabiliana na janga la COVID-19 baada ya kupuuzia kwa muda mrefu. Je, visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi vinaelekea kukubali chanjo kabla ya ibada ya Hijja kuanza?

Hofu ya Waislamu wa Zanzibar na pengine Tanzania kwa ujumla inatokana na utawala wa nchi ya Saudi Arabia kuweka sharti kwamba Waislamu watakaoruhusiwa kuingia na kufanya hijja ni wale tu waliopata chanjo kamili dhidi ya virusi vya ambavyo bado vinaitesa dunia kwa kiwango kikubwa.

Hofu inatokana na muda uliosalia hadi Hija

Akihutubia katika baraza la Eid Ijumaa iliyopita Rais wa Zanzibar DkHussein Ali Mwinyi aliwaaambia waislamu wanaojindaa kwenda hijja mwaka huu kuwa serikali inasubiri ufafanuzi zaidi kutoka serikali ya Saudi Arabia kuhusu sharti la chanjo, lakini serikali itahakikisha inawasaidia kutimiza matakwa hao na kuwataka wajiandae.

Afrika Sansiba Amtseinführung Staatsministerin
Rais wa Zanzibar dokta Hussein Mwinyi (kushoto)Picha: Salma Said/DW

Hata hivyo hofu ya waislam wa nchini hapa inatokana na muda uliobaki wa kujiandaa ikiwa pamoja na kupata chanjo mara mbili kabla ya safari kuwa mdogo.

Tangazo la Rais Mwinyi lilitafsiriwa kama kwamba Zanzibar inataka kuchukuwa muelekeo mpya kuhusiana na kukabiliana na janga la COVID-19 kwa kuruhusu chanjo, ambazo hadi sasa bado hazijawekwa wazi kote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na msimamo wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Marehemu John Magufuli juu ya kadhia nzima ya virusi vya corona.

Hatua zilizochukuliwa na magufuli kuikabili corona ziliiathiri Zanzibar pia

Hata hivyo, endapo kilichotafsiriwa sivyo hasa kilivyomaanisha, baadhi ya wananchi wanaona kwamba matumaini yao ya kwenda Hijja huenda yakavia.

Tansania l Präsident Magufuli ist gestorben, Archiv
Rais wa zamani wa Tanzania marehemu John MagufuliPicha: Sadi Said//REUTERS

Hatua za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Marehemu Rais Magufuli katika kulikabili janga la virusi vya corona ziliathiri pia upande wa Zanzibar, licha ya kwamba masuala ya afya si katika mambo ya Muungano, na Zanzibar haikuchukuwa muelekeo tafauti kwa janga hilo la kilimwengu. Endapo sasa hatua hizo zitabadilika ama la, ni jambo la kungoja na kuona.