Wawili wauawa Ukraine baada ya kushambuliwa kwa droni
20 Januari 2025Hayo yameripotiwa na vyombo vya habari vya serikali ya Urusi.
Gavana wa mkoa huo aliyewekwa rasmi na serikali ya Urusi amesema kuwa vikosi vya Ukraine vilifyatua "mabomu mengi" karibu na shule katika mji wa Bekhtery wakati wanafunzi na walimu walipokuwa wakienda masomoni na kwamba watoto walikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa.
Urusi na Ukraine zimezidisha mashambulio baina yao katika miezi ya hivi karibuni katika mzozo wao wa karibu miaka mitatu kabla ya kuapishwa kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump leo Jumatatu. Trump alisema kwamba anataka kuvimaliza vita hivyo hivi karibuni.
Katika hatua nyingine maafisa watatu wa ngazi za juu wa jeshi la Ukraine wanashikiliwa kwa madai ya "kutochukua hatua" na kuruhusu vikosi vya Urusi kuteka sehemu za eneo la mashariki la Kharkiv mwaka uliopita, waendesha mashtaka wameyasema hayo leo Jumatatu.