1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wawakilishi wa UN na ECOWAS wawasili Guinea kutuliza vurugu

26 Oktoba 2020

Wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na kanda ya maendeleo ya uchumi magharibi ya Afrika, Ecowas, wawasili nchini Guinea baada ya uchaguzi wa rais wenye utata kuzusha vurugu

https://p.dw.com/p/3kRrY
Guinea Anhänger von Oppositionsführer Cellou Dalein Diallo feiern den vermeintlichen Wahlausgang
Picha: John Wessels/AFP

Waziri wa Mambo ya kigeni wa Guinea Mamadi Toure amesema ujumbe wa taasisi hizo umewasili kwa juhudi za kidiplomasia bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Ujumbe huo unajumuisha rais wa halmashauri kuu ya jumuiya ya ECOWAS Jean-Claude Kassi Brou na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa kanda ya Afrika Magharibi Mohamed Ibn Chambas.

Rais Alpha Konde alipata ushindi kwenye uchaguzi wa ushindani mkali uliofanyika Oktoba 18 hatua inayomwezesha kuanza muhula wa tatu madarakani ambao umekuwa ukipingwa kwa maandamano ya umma.

Hata hivyo mpinzani wake mkuu Cellou Dalein Diallo aliyapinga matokeo hayo na kujitangaza kuwa mshindi, uamuzi uliochochea makabiliano kati ya wafuasi wake na vikosi vya usalama yaliyosababisha vifo vya watu 10.