1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Wawakilishi wa Marekani kukutana na wa utawala wa Taliban

27 Julai 2023

Maafisa wa Marekani watakutana na wawakilishi wa Taliban na wataalam wa masuala ya teknolojia katika wizara za Afghanistan mjini Doha wiki hii kujadiliana masuala ya kiuchumi, usalama na haki za wanawake.

https://p.dw.com/p/4USan
Afghanistan Taliban-Vertreter führen in Doha Gespräche mit US-amerikanischen und europäischen Delegierten
Picha: Stringer/REUTERS

Katika taarifa iliyotolea, naibu msemaji katika wizara hiyo ya ulinzi ya Marekani, Vedant Patel, amesema mwakilishi maalum wa Marekani nchini Afghanistan, Thomas West, na mwakilishi maalum wa haki za wanawake na wasichana, Rina Amiri, ndio watakaokutana na wawakilishi wa Taliban.

Soma zaidi: Wajumbe wa Afghanistan wakutana na Taliban

Hata hivyo, Patel amedai kuwa mazungumzo hayo ya Doha hayaashirii kwa njia yoyote ile Marekani kuitambua serikali ya Taliban.

Hakuna nchi duniani iliyoutambua rasmi utawala wa Taliban tangu kundi hilo liliporudi madarakani nchini Afghanistan mwaka 2021 kufuatia hatua ya majeshi ya Marekani kuondoka nchini humo baada ya miaka 20 ya mapambano.