Waislamu wakusanyika kwa ajili ya ibada mlima Arafa
15 Juni 2024Matangazo
Waumuni hao kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni watakwea mlima huo wenye futi 230, ikiwa ni takriban kilometa 20 kutoka mji Mtakatifu kwa Waislamu wa Makka ambako Mtume Muhammad anaaminika kutoa mahubiri yake ya mwisho.
Joto la jangwani majira ya kiangazi linatarajiwa kufikia nyuzi joto 43 katika kipimo cha Selsiasi, na kuwa chagizo miongoni mwa wazee katika siku hii muhimu na kudurusu Kurani.
Soma pia:Mahujaji wa Kiislamu wajiandaa kwa ibada rasmi ya Hija
Mamlaka ya Saudia imewataka mahujaji kunywa maji mengi na kujikinga na jua.
Ibada ya hija ni miongoni mwa nguzo tano katika dini ya Kiislamu na hufanywa kwa wale wenye uwezo kiuchumi na afya njema.