1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watuhumiwa wa ugaidi wakamatwa Ujerumani

2 Januari 2024

Maafisa wa usalama nchini Ujerumani wamewakamata watu wengine wawili wanaotuhumiwa kupanga njama za kulishambulia kanisa kuu la mji wa Cologne katika mkesha mwaka mpya.

https://p.dw.com/p/4an7h
Polisi wa jimbo la NRW la Ujerumani
Polisi wa jimbo la NRW la UjerumaniPicha: Christoph Reichwein/dpa/picture alliance

Maafisa wa usalama nchini Ujerumani wamewakamata watu wengine wawili wanaotuhumiwa kupanga njama za kulishambulia kanisa kuu la mji wa Cologne katika mkesha mwaka mpya.

Mtuhumiwa mmojawapo ni mwenye umri wa miaka 25 kutoka Tajikistan ambaye alikamatwa kabla ya Krismasi. Mwengine alitiwa mbaroni siku ya Jumapili.

Polisi ya mjini Colonge imesema watu hao wanaweza kushikiliwa kwa zaidi ya siku 14 ili kuhojiwa.

Watuhumiwa wengine watatu waliokamatwa siku ya Jumapili wameachiwa. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, watu hao wanadaiwa kutaka kufanya mashambulizi nchini Ujerumani, Austria na Uhispania kwa niaba ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS, tawi la Afghanistan.