1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Watu wengine 9 waokolewa tetemeko la Taiwan

5 Aprili 2024

Watu tisa wameokolewa kutoka kwenye mapango ya mashariki ya milima ya Taiwan, huku wengine wawili waliopatikana wakihofiwa kufariki dunia.

https://p.dw.com/p/4eSJr
Taiwan | Tetemeko la ardhi
Miongoni mwa majengo yaliyobomolewa na tetemeko la ardhi la Jumatano nchini Taiwan.Picha: Chiang Ying-ying/AP Photo/picture alliance

Vikosi vya uokoaji vya Taiwan vinaendelea na juhudi za kuwatafuta watu wengine 18 waliokwama kwenye eneo moja la milimani baada ya tetemeko kubwa la ardhi kukipiga kisiwa hicho siku ya Jumatano (Aprili 3).

Siku ya Ijumaa (Aprili 5), Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Japana, Yoko Kamikawa, aliahidi kuwa nchi yake ingelitowa dola milioni moja ya misaada kwa Taiwan ili kusaidia shughuli za uokoaji.

Soma zaidi: Tetemeko la ardhi Taiwan lauwa watu 7 na kuwajeruhi 800

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida kupitia mitandao ya kijamii siku ya Jumatano aliandika kwamba nchi yake ilikuwa tayari kutoa msaada na kuitaja Taiwan kama "rafiki na jirani muhimu".

Idadi rasmi ya watu waliofariki dunia kutokana na tetemeko la Taiwan lenye ukubwa wa 7.4 kwa kipimo cha Richter imefikia 10, lakini serikali katika Kaunti ya Hualien, eneo lililoathiriwa zaidi, inasema watu wawili walipatikana kwenye njia ya kupanda mlima bila "dalili za kuwa hai."