Watu wawili wanyongwa kwa kushambulia eneo takatifu Iran
8 Julai 2023Tukio hilo la Oktoba 26 ambalo kundi la itikadi kali linalojulikana kama "Sunni Muslim extrimist Islamic State" lilidai kuhusika nalo lilisababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi wengine 30.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Iran IRNA, hukumu hiyo ya kifo imetekelezwa leo asubuhi ambapo wawili hao walinyongwa karibu na eneo hilo takatifu kwenye mji wa Shiraz ambao ni makao makuu ya mkoa wa Fars.
Soma zaidi:Amnesty: Idadi ya watu walionyongwa iliongezeka mwaka 2022
Watu hao waliotambulishwa kwa majina ya Ramez Rashidi na Naeem Hashem Qatali walihukumiwa adhabu hiyo mnamo mwezi Machi mwaka huu kwa makosa ya rushwa, uasi wa kutumia silaha na kwa kujihusisha na vitendo vinavyotishia usalama wa taifa. Washukiwa wengine watatu katika kesi hiyo walihukumiwa kifungo cha miaka 15 na 25 gerezani.