1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiBurkina Faso

Watu wawili wafungwa Burkina Faso kwa kushambulia mgahawa

3 Januari 2025

Mahakama moja nchini Burkina Faso imewahukumu watu wawili kifungo cha maisha jela, baada ya kukutwa na hatia ya kuushambulia mgahawa wa Kituruki katika mji mkuu Ouagadougou, mwaka 2017.

https://p.dw.com/p/4omoV
Waliouawa ni pamoja na raia 10 wa Burkina Faso na raia tisa wa kigeni
Waliouawa ni pamoja na raia 10 wa Burkina Faso na raia tisa wa kigeniPicha: SIA KAMBOU/AFP via Getty Images

Mahakama moja nchini Burkina Faso imewahukumu watu wawili kifungo cha maisha jela, baada ya kukutwa na hatia ya kuushambulia mgahawa wa Kituruki katika mji mkuu Ouagadougou, mwaka 2017. Maafisa walisema jana kuwa shambulizi hilo lilisababisha mauaji ya watu 19.

Watu wawili waliokuwa na bunduki waliwafyetulia risasi watu katika mgahawa wa Aziz Istanbul, kwenye barabara kuu ya Ouagadougou, Agosti 2017. Ofisi ya kupambana na ugaidi ilisema washambuliaji hao walikamatwa wakati wa oparesheni mwaka 2018, kufuatia upepelezi.

Washambuliaji wengine wawili waliuawa na vikosi vya usalama wakati wa makabiliano katika shambulizi hilo. Waliouawa ni pamoja na raia 10 wa Burkina Faso na raia tisa wa kigeni.

Kama ilivyo kwa mataifa mengine ya Ukanda wa Sahel ya Mali na Niger, ambayo yanaongozwa na utawala wa kijeshi, Burkina Faso imekuwa ikikabiliana na ongezeko la mashambulizi ya wapiganaji wa jihadi.