Watu watano wauawa katika shambulio Somalia
7 Novemba 2022Shambulio la bomu la kujitoa mhanga lilitokea kwenye lango la kuingilia kwa kambi watu watano walikufa katika mlipuko huo na wengine zaidi ya kumi walijeruhiwa.
Hakuna taarifa rasmi iliyo tolewa na serikali kuhusu shambulio linalodaiwa kufanywa na al-Shabaab, ambao wapiganaji wao wenye mafungamano na al-Qaeda wameongeza mashambulizi nchini Somalia tangu Rais Hassan Sheikh Mohamud alipoingia madarakani mwezi Mei na kuapa kwa "vita kamili" dhidi ya wanajihadi
Shambulio hilo lilitokea katika makutano hayo ambapo lori lililokuwa limejaa vilipuzi lili lipuka Oktoba 14,2017 na kuua watu 512 , na kujeruhi wengine zaidi ya mia mbili tisini. Mwezi Agosti, kundi hilo lilivamia hoteli maarufu ya Hayat mjini Mogadishu kwa takriban saa thelathini, na kuua watu ishirini na moja na kuwajeruhi wengine 117.
Waasi hao waliotaka kuiangusha serikali dhaifu, walifurushwa kutoka mji mkuu wa Mogadishu, mwaka 2011, na kikosi cha Umoja wa Afrika. Lakini kundi hilo bado lina dhibiti maeneo makubwa ya nchi na linaendelea kufanya mashambulizi mabaya dhidi ya malengo ya kiraia, kisiasa na kijeshi.