Watu watano wafariki Tanzania baada ya mripuko wa Marburg
22 Machi 2023Matangazo
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema visa hivyo vilitambuliwa katika mkoa wa magharibi wa Kagera na serikali imefanikiwa kuudhibiti kusambaa katika maeneo mengine.
Waziri huyo amesema mpaka sasa jumla ya watu walioambukizwa na wanane.
Kirusi cha Marburg, kinasababisha maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, kutapika, kuharisha na kutokwa damu sehemu mbalimbali za mwili.
Watu wanaweza kuambukizwa kwa kugusa majimaji ya mwili au watu walioambukizwa.
Mapema mwaka huu, Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO lilithibitisha mripuko wa Marburg katika Guinea ya Ikweta Afrika Magharibi.
Kenya na Uganda ziko katika hali ya tahadhari kutokana na visa vya karibuni nchini Tanzania