Watu wanane wauawa katika mlipuko wa bomu Syria
31 Machi 2024Shirika linalofuatilia Haki za Binaadamu la Syria limesema watu zaidi ya 20 walijeruhiwa baada ya bomu lililokuwa ndani ya gari kulipuka katikati ya soko hilo maarufu la mji wa Azaz katika mkoa wa Aleppo.
Hakuna kundi lililodai mara moja kuhusika na shambulizi hilo. Uturuki ilianzisha operesheni za kijeshi nchini Syria, nyingi zikiwalenga wanamgambo wa Kikurdi ambao Ankara inawahusisha na chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi - PKK, ambacho kimeendesha uasi wa miongo kadhaa dhidi ya taifa la Uturuki.
Wanajeshi wa Uturuki na washirika wao nchini Syria wanadhibiti maeneo makubwa ya mpaka wa kaskazini magharibi, ikiwemo miji kadhaa mikubwa kadhaa kama Azaz. Rais Bashar al-Assad alichukua tena udhibiti wa theluthi mbili ya nchi, kwa msaada wa washirika wake Urusi, Iran na wanamgambo wa Hezbollah wa nchini Lebanon.