1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiCanada

Watu sita wafariki katika ajali ya ndege Canada

24 Januari 2024

Watu sita wamekufa baada ya ndege ndogo ya abiria iliyokuwa imewabeba wafanyikazi kuwapeleka kwenye mgodi kaskazini mwa Canada kuanguka muda mfupi tu baada ya kupaa angani.

https://p.dw.com/p/4bbgK
Ndege ya shirika la Air Canada ikiwa angani baada ya kuondoka kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pearson, Toronto.
Ndege ya shirika la Air Canada ikiwa angani baada ya kuondoka kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pearson, Toronto. Picha: Carlos Osorio/REUTERS

Kwa mujibu wa vyanzo, mtu mmoja amenusurika kifo japo hali yake ya kiafya bado haijawekwa wazi kwa umma.

Vikosi vya usalama vimetumwa katika maeneo ya Kaskazini Magharibi kulikotokea ajali hiyo ili kusaidia katika oparesheni za uokoaji.

Kampuni inayosimamia ndege hiyo imeeleza kuwa, ndege hiyo aina ya Jetstream iliyokuwa imebeba wafanyikazi kuelekea kwenye mgodi ilianguka yapata kilomita 1.1 baada ya kupaa.

Kutokana na ajali hiyo, safari zote za ndege kutoka Fort Smith zimesitishwa kwa muda. Bodi ya usalama wa anga ya Canada imeunda kikosi maalum kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.