1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUbelgiji

Watu sita hatiani kwa mauaji ya Brussels ya mwaka 2016

26 Julai 2023

Mahakama moja nchini Ubelgiji imewakuta na hatia ya mauaji wanaume sita kwa kuhusika katika mashambulizi ya Brussels mwaka 2016. Watu 32 waliuawa katika mashambulizi hayo na wengine zaidi ya 300 walijeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4UOab
Ubelgiji yaanza kesi ya mashambulizi ya mabomu mjini Brussels Novemba 30, 2022
Laurence Massart- Jaji wa mahakama nchini Ubelgiji Picha: Stephanie Lecocq/AFP

Miongoni mwa waliokutwa na hatia ni Salah Abdeslam, raia wa Ufaransa na Mohamed Abrini raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Morocco. Abdeslam tayari anatumikia kifungo cha maisha gerezani nchini Ufaransa, kutokana na kuhusika katika mashambulizi ya Paris, mwaka 2015, ambayo yaliwaua watu 130.

Hukumu kutolewa kwa utaratibu tofauti ifikapo mwezi Septemba

Uamuzi huo wa mahakama unaufunga ukurasa wa kesi kubwa zaidi kuwahi kusikilizwa katika historia ya mahakama ya Ubelgiji. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mwezi Desemba. Kufuatia uamuzi huo, hukumu itatolewa kwa utaratibu tofauti ifikapo mwezi Septemba. Kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS lilikiri kuhusika katika mashambulizi hayo.