1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 9,000 wauawa Sudan

16 Oktoba 2023

Mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths, amesema vita vya Sudan, ambavyo vimedumu kwa miezi sita sasa, vimewaua watu wapatao 9,000.

https://p.dw.com/p/4XZXs
Sudan | die Generäle Abdel Fattah Abdelrahman al-Burhan und Mohamed Hamdan Dagalo
Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Griffiths alisema hayo siku ya Jumapili (Oktoba 15) akieleza zaidi kuwa vita hivyo kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha Msaada wa Dharura (RSF), vimesababisha moja kati ya migogoro mibaya ya kibinaadamu katika historia ya hivi karibuni.

Sudan imezongwa na machafuko tangu katikati ya mwezi Aprili, wakati mvutano kati ya mkuu wa majeshi, Jenerali Abdel-Fattah Burhan, na kamanda wa kikosi cha RSF, Jenerali Mohamed hamdan Dagalo, ulipogeuka vita vya wazi.

Soma: Sudan: UN inajitahidi kuwafikia watu milioni 18 wanaohitaji msaada

Kulingana na Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM), zaidi ya watu milioni 4.5 wamekuwa wahamiaji wa ndani nchini Sudan, huku wengine zaidi ya milioni 1.2 wakikimbilia nchi jirani.

Griffiths amesema pia kuwa mapigano hayo yamewaacha watu milioni 25, hiyo ikiwa zaidi ya nusu ya idadi jumla ya Wasudan wanaohitaji misaada ya kibinaadamu.