1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Watu 90 wafariki katika operesheni ya Israel Al Shifa

20 Machi 2024

Jeshi la Israel limedai hii leo kuwaua watu 90 wenye silaha na kuwakamata wengine 160 katika operesheni yake kwenye hospitali kubwa ya Ukanda wa Gaza ya Al-Shifa.

https://p.dw.com/p/4dvRq
Wanajeshi wa Israel katika operesheni ya ardhini Khan Younis
Wanajeshi wa Israel katika Ukanda wa GazaPicha: Ohad Zwigenberg/AP/picture alliance

Israel inadai kuwa wapiganaji wa Hamas hutumia mahandaki ya hospitali hiyo kujificha na kuratibu mashambulizi yao.

Mara kadhaa, Hamas na wahudumu wa afya wamekuwa wakikanusha kuwa hospitali hiyo hutumiwa kwa madhumuni ya kijeshi au kuwahifadhi wapiganaji.

Hayo yakijiri, familia za mateka na wanaharakati wameandamana na kuzuia barabara kuu mjini Tel Aviv wakiishinikiza serikali ya Israel kufikia makubaliano yatakayowezesha mateka zaidi kuachiwa huru. Ayala Metzger ni mwanafamilia wa mmoja wa mateka walioshikiliwa huko Gaza.

Kuna wazee huko Gaza, waliotekwa byara pamoja wanajeshi, watoto wachanga na wanawake. Tunataka warudi nyumbani, hatutaki wafe. Serikali ya Israeli inapaswa kutimiza wajibu wake. Tunaitaka ifikie makubaliano haraka iwezekanavyo. Serikali ihakikishe inaidhibiti hali hiyo, na kuwarejesha japo baadhi yao, haraka iwezekanavyo," alisema Metzeger.

Watu wengine 28 wameuawa kufuatia mashambulizi ya Israel katika kambi ya wakimbizi ya Deir al-Balah huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akisema pia kuwa analenga kuanzisha operesheni huko Rafah.

Kwa taarifa hii na nyingine zaidi, tazama chaneli yetu ya YouTube.