1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Watu 50 wauawa katika mashambulizi ya kundi la RSF Sudan

Saleh Mwanamilongo
26 Oktoba 2024

Watu wapatao 50 wameuawa katika shambulio la wanamgambo wa Sudan ambao wamezingira na kuvamia vijiji katika jimbo la al-Jazira, Mashariki mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4mGkv
South Sudanese RUganda Kaya
Picha: Sumy Sadurni/picture alliance

Wanaharakati wanaoratibu misaada nchini Sudan wameliambia shirika la habari la AFP kwamba vijiji vya al-Sariha na Azraq vimekuwa vikishambuliwa na wanamgambo wa RSF tangu Ijumaa asubuhi.

Taarifa zimesema katika kijiji cha al-Sariha pekee, shambulio la RSF liliua watu 50 na kujeruhi zaidi ya 200. Ni vigumu kuthibitisha idadi hiyo ya vifo kutokana na ukosefu wa mawasiliano na eneo hilo.

Jana Ijumaa, muungano wa madaktari wa Sudan ulitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kushinikiza kuwepo kwa njia salama za kibinadamu katika vijiji ambavyo vinakabiliwa na kile walichoita kuwa ni "mauaji ya halaiki" yanayofanywa na wanamgambo wa RSF.

Vita nchini Sudan vimeua makumi ya maelfu ya watu, huku baadhi ya makadirio yakisema watu 150,000 wamekufa.