1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 50 wafunguliwa mashitaka kwa mauaji ya rais Moise

20 Februari 2024

Jaji mmoja nchini Haiti ambaye anafuatilia uchunguzi wa mauaji ya Rais Jovenel Moise, amewafungulia mashtaka takriban watu hamsini, akiwemo mjane wa rais na waziri mkuu wa zamani.

https://p.dw.com/p/4ccJH
Haiti I rais Jovenel Moise
Watu 50 wamekamatwa wakihusishwa na mauaji ya rais wa Haiti Jovenel Moise Picha: Matias Delacroix/AP/picture alliance

Jaji Walther Wesser Voltaire, ametoa waraka wenye kurasa 122 unaomshtaki mjane wa rais Martine Moise kwamba alikula njama na Waziri Mkuu wa zamani Claude Joseph ya kumuua rais wa taifa hilo la Caribbean ili mwanamke huyo aweze kuchukua nafasi hiyo.

Waziri mkuu huyo wa zamani amesema hatua hiyo imechochewa kisiasa na kwamba mtawala wa sasa wa Haiti Ariel Henri anajaribu kuwakandamiza wapinzani kwa kutumia vyombo vya sheria.

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya rais wa Haiti akamatwa

Rais Moise aliuawa kwa kupigwa risasi huku mkewe akijeruhiwa baada ya kuvamiwa katika makazi yake katika mji mkuu Port-au-Prince usiku wa Julai 7, mwaka 2021.