Watu 42 wauwawa na waasi wa ADF nchini Kongo
14 Juni 2024Kiongozi wa Bapere, Makere Sivikunula Mwendovwa, alitangaza idadi hiyo ambayo huenda ikaongezeka kwani, kila wanapofanya mauwaji wanaendelea kuwauwa watu wengine wakielekea katika eneo jengine.
Mauwaji katika kijiji cha Maikengo wilayani Lubero, yanafuatia yale ya Cantine, magharibi mwa wilaya ya Beni, ambako wapiganaji wa ADF waliwauwa watu wasiopungua mia mbili wiki iliyopita.
Idadi ya vifo yaongezeka hadi 41 kufuatia shambulio mashariki mwa Kongo
Mashambulizi yanayofanywa na ADF katika mikoa ya Kivu ya Kaskazini pamoja na Ituri, yamegharimu maisha ya maelfu ya raia nchini Kongo.
Ili kukabiliana na mauwaji pamoja na vita vya M23 katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini, mkuu wa majeshi ya Congo jenerali Tshiwewe Songisa alikutana jana mjini Goma kwa mazungumzo maalumu na makamanda wa operesheni katika mkoa huu.