Manusura 41 wa maporomoko mbioni kuokolewa India
28 Novemba 2023Tukio lililotokea majuma mawili yaliopita. Maafisa wanasema juhudi ya kuchimba kuwajongelea inaendelea na upo uhakika wa kiwafikia.
Wafanya kazi hao wa ujira wa kipato cha chini, kutoka katika jimbo duni zaidi nchini India, wamekwama katika eneo la baranara la ya chini ya urefu wa kilometa 4.5, tangu ya kuporomoka kwa barabarabara hiyo Novemba 12. Kikosi cha waokozi jana Jumatatu kilipasua miamba na mawe kwa kutumia nyenzo za mikononi kwa urefu wa futi tatu, ikiwa baada ya mashine kushindswa kufanya kazi. Kwa hatua hiyo maafisa wanasema ni ishara njema.
Waziri Mkuu wa Jimbo la Uttarakhand, Pushkar Singh Dhami amesema kulikuwa na changamoto ya kukabiliana na vyuma katika juhudi hiyo lakini kwa wakati huu imepungua. Na sasa wanakabiliana na zege ambalo linakatwa.
Jitihada ya matumaini ya kuwakoa wote 41.
Awali akiwa katika eneo la tukio mtaalamu katika ujenzi wa baraabara za chini ya ardhi, raia wa Australia, Chris Cooper alisema "Uokozi unakwenda vizuri. Tumechimba mita 50, tunaweza sema ni takribani mita 5.6 kufika. Tumeweka bomba lingine. Kwa hivyo leo tunatarajia matokeo mazuri."
Watu hao walionasa, wanapata vyakula, maji,mwanga, hewa safi ya oksijen kwa kupitia bomba lakini juhudi za kuchimba eneo lilifunikwa na maporomoko katika barabara hiyo na kuwaokoa kwa kutumia mashine za kuchimbia imekuwa changamoto kutokana na kuharibika mara kwa mara.
Lakini jana Jumatatu, waokozi waliwatumia wachimbaji wenye kutumia zana za mikono, ambao wanatumia mbinu za kizamani, hatarishi na zenye utata ambazo kwa kawaida zinatumika katika uchimbaji wa makaa ya mawe. Jamii hii hiyo ya wachimbaji inajulikana sana nchini India kama "rat miners" kutokana na namna yao ya uchimbaji kufanana na panya.
Ndungu ya walionasa wapiga kambi katika eneo la tukio.
Duru zinaleza Jamaa wa baadhi ya watu hao walionasa 41 ambao wamekuwa wakipiga kambi karibu na eneo la ajali huku wakiwa na mavazi na mabegi ya ndugu zao hao wakiwa tayari kuwapokea na punde watakapotolewa na kuwapeleka hospitali ambayo ipo umbali wa kilometa 30 kutoka katika eneo hilo.
Eneo hilo la barabara ya chini ya ardhi ni sehemu ya mradi wa barabara kubwa ya Char Dham, iliyogharimu dola bilioni 1.5, ukiwa moja kati ya miradi ya muhimu ya Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, wenye lengo la kuyaunganisha maeneo manne ya hija kwa imani ya Kihindu, ambayo ina mtandao wa barabara ya urefu wa kilometa 890.
Soma zaidi: India yapitisha sheria inayotoa fursa wanawake kupata viti bungeni
Mamlaka haijasema kilichosababisha eneo hilo la barabara kuporomoka lakini kimsingi linakabiliwa na maporomoko ya ardhi, matetemeko ya ardhi na mafuriko.
Chanzo: AFP