1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Watu 38 wafa kwa mafuriko China

21 Juni 2024

Idadi ya vifo kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi kusini mwa China imeongezeka na kufikia watu 38.

https://p.dw.com/p/4hMwP
China | mafuriko Guangdong
Matokeo ya mafuriko katika jimbo la Guangdong nchini China.Picha: Lu Hanxin/Xinhua/AP/picture alliance

Mvua zilizonyesha wiki hii katika jiji la Meizhou mkoani Guangdong zilisababisha mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyoharibu mazao, maelfu ya nyumba za makazi, barabara na kuvuruga huduma za mawasiliano na umeme.

Soma zaidi: Watu 36,000 wahamishwa kufuatia mafuriko makubwa mkoa wa Fujian, China

Licha ya kuwa China imejaribu kwa miaka mingi kudhibiti idadi ya vifo vitokanavyo na mafuriko, mabadiliko ya hali ya hewa yameiweka nchi hiyo katika hatari ya kukumbwa na aina mbalimbali za majanga ya asili. 

Katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu, China ilipata hasara ya moja kwa moja ya kiuchumi ya dola bilioni 3.27, kutokana na maafa ya asili, ikiwa ni pamoja na mafuriko, ukame, matetemeko ya ardhi na baridi kali.