JamiiBrazil
Watu 36 wafariki kutokana na mafuriko Brazil
20 Februari 2023Matangazo
Maafisa wamesema watu 35 wamekufa katika mji wa Sao Sebastiao kusini mashariki mwa Brazil, na mmoja amekufa katika mji wa Ubatuba.
Wafanyakazi wa uokozi wakisaidiwa na helikopta, walikuwa wanawatafuta waathirika zaidi. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, watoto ni miongoni mwa watu waliokufa.
Gavana wa Sao Paulo, Tarcisio de Freitas, ametangaza hali ya hatari kwenye manispaa tano zilizoathiriwa.
Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, leo anatarajiwa kulizuru eneo hilo. Makaazi ya zaidi ya watu 330 yameharibiwa na barabara kadhaa zimefungwa kutokana na mvua hizo zilizoanza kunyesha siku ya Jumamosi.