1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaNiger

Watu 339 wafa kwa mafuriko Niger

9 Oktoba 2024

Watu 339 wamekufa baada ya mvua za msimu kusababisha mafuriko nchini Niger, na wengine zaidi ya milioni 1.1 kukosa makaazi tangu mwezi Juni.

https://p.dw.com/p/4laOS
Watu 339 wamekufa baada ya mvua za msimu kusababisha mafuriko nchini Niger
Watu 339 wamekufa baada ya mvua za msimu kusababisha mafuriko nchini NigerPicha: BOUREIMA HAMA/AFP

Mwezi uliopita, waziri wa mambo ya ndani alisema watu 273 walikufa na wengine zaidi ya 700,000 waliathiriwa na hali mbaya ya hewa kwenye taifa hilo la Sahel.

Shirika la habari la serikali, ANP, liliripoti jana kuwa hadi kufikia Septemba 23, mafuriko yamewaathiri zaidi ya watu milioni 1.1, na kusababisha vifo 339, na kuwajeruhi wengine 383.

ANP ililinukuu shirika la ulinzi wa raia. Maeneo kote nchini humo yameathiriwa na mafuriko hayo, ukiwemo mji mkuu, Niamey, ambako watu tisa walifariki. Mafuriko hayo pia yamesababisha hasara kubwa ya vifaa, mifugo na chakula.