Watu 30 wauwawa katika mashambulizi ya anga Sudan
10 Septemba 2023Matangazo
Kulingana na moja ya makundi ambayo yalikuwa yakiandaa maandamano ya kuunga mkono demokrasia na sasa yanatoa msaada wakati wa vita, ndege za kijeshi zilishambulia soko la Qouro mwendo wa saa moja na robo asubuhi.
Soma pia: Shambulio la anga lawaua raia 20 huko Sudan
Kamati ya hospitali ya Bashair imetoa "wito wa dharura" kwa wataalamu wote wa afya katika eneo hilo kufika hospitali ili kusaidia kutibu "idadi inayoongezeka ya watu waliojeruhiwa".
Tangu Aprili 15, Sudan imekuwa ikikabiliwa na vita vya kutisha vinavyohusisha jeshi la kawaida dhidi ya kikosi cha wapiganaji wa akiba kilichoasi cha RSF huku juhudi za kimataifa zikishindwa kufikia usitishaji mapigano katika mzozo huo.