JangaAfghanistan
Afghanistan: Watu 21 wafariki katika ajali ya barabarani
17 Machi 2024Matangazo
Ajali hiyo ilitokea katika barabara kuu ya Herat-Kandahar katika wilaya ya Greshk. Polisi wa eneo hilo wamesema ajali hiyo ilisababishwa na basi la abiria kugongana na pikipiki, na kisha dereva wa basi hilo kupoteza udhibiti wa gari lake na kugonga lori la mafuta na kusababisha moto mkubwa.
Watu 11 wapo katika hali mbaya na wanapatiwa matibabu katika hospitali mkoani humo.
Ajali za barabarani zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara nchini Afghanistan, ambako maelfu ya watu hufariki kila mwaka kutokana na ubovu wa barabara, na matengenezo hafifu pamoja na ukosefu wa umakini katika uendeshaji wa vyombo vya usafiri.