SiasaEcuador
Temeko la ardhi laua watu 15 nchini Ecuador na Peru
19 Machi 2023Matangazo
Watafiti wa Jiolojia wa Marekani wamesema tetemeko hilo lilipiga pwani ya Ecuador katika mkoa wa Guayas.
Idadi kubwa ya vifo kufuatia tetemeko hilo imeshuhudiwa nchini Ecuador ambapo rais wa nchi hiyo Guillermo Lasso akitoa wito wa utulivu na kuyatembelea majimbo yaliyoathiriwa zaidi ya El Oro na Azuay.
Ecuador na Peru zinapatikana katika sehemu inayojulikana kama "Gonga la Moto la Pasifiki", ambalo hukumbwa mara kwa mara na matetemeko ya ardhi kutokana na kuhifadhi takriban volkano 128.