Watu 143 wafariki dunia Brazil kutokana na mafuriko
13 Mei 2024Mamlaka nchini Brazil imesema watu wengine 125 hawajulikani waliko katika jimbo hilo la kusini mwa Brazil ambapo viwango vya maji kwenye mito inaripotiwa kupanda. Idara ya hali ya hewa imesema mvua zinazoendelea kunyesha "zinatia wasiwasi."
Mnamo siku ya Jumamosi, serikali ilitangaza kitita cha dola bilioni 2.34 kwa matumizi ya dharura ili kushughulikia janga hilo ambalo limesababisha zaidi ya watu 538,000 kuyahama makazi yao.
Soma pia: Mafuriko yaua watu 75 na kujeruhi wengine 155 Brazil
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amesema serikali kuu itajenga upya miundombinu yote iliyoharibiwa na mvua katika jimbo hilo la Rio Grande do Sul.
Kwa upande wake, Rais Joe Biden wa Marekani amesema utawala wake unawasiliana na Brazil kwa lengo la kutoa msaada kwa waathiriwa wa mafuriko.