1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Watu 13 wafariki baada ya maporomoko ya ardhi Uganda

28 Novemba 2024

Karibu watu 13 wamekufa mashariki mwa Uganda baada ya maporomoko ya ardhi kuzifukia nyumba 40 katika vijiji sita. Shirika la Msalaba Mwekundu la Uganda limesema miili 13 imepatikana na juhudi za uokozi zinaendelea.

https://p.dw.com/p/4nXI1
Uganda | Bulambuli
Watu 13 wafariki baada ya maporomoko ya ardhi kufukia nyumba 40 mashariki mwa UgandaPicha: Nakasiita/AP Photo/picture alliance

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa maafisa wanatarajia idadi ya vifo huenda ikapanda hadi watu 30. Maporomoko hayo ya ardhi yalitokea baada ya mvua kubwa kunyesha jana usiku katika wilaya ya Bulambuli iliyoko eneo la milimani. Eneo hilo kumbukwa na maporomoko ya ardhi ya mara kwa mara.

Kiasi ya watu 30 wahofiwa kufa kwenye maporomoko ya ardhi Uganda

Gazeti la Daily Monitor limeripoti kuwa nyingi ya miili iliyopatikana mpaka sasa ni ya watoto wadogo. Picha na vidio za watu wakichimba kwenye matope kuwatafuta waathirika zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Baadhi nyumba zilifukiwa kabisa na matope. Ofisi ya waziri mkuu ilitoa tahadhari ya maafa jana ikisema kuwa mvua kubwa kote nchini humo ilikuwa imeharibu barabara nyingi.