1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 10 wauawa na 25 wajeruhiwa katika ajali ya basi Uturuki

9 Agosti 2024

Takriban watu kumi wamefariki na wengine 25 wamejeruhiwa leo baada ya basi la abiria kugonga nguzo ya barabara kuu katikati mwa Uturuki.

https://p.dw.com/p/4jIOE
Slowakei I Zugunglück
Picha: Henrich Misovic/AP/picture alliance

Shirika la utangazaji la serikali TRT limeripoti kuwa ajali hiyo imetokea leo alfajiri karibu na mji mkuu wa Ankara, katika wilaya ya Polatli.

Gavana wa Ankara Vasip Sahin ameliambia shirika la habari la TRT kuwa, dereva wa basi hilo ni miongoni mwa waliopoteza maisha.

Basi hilo lilikuwa linatokea mji wa pwani ya Aegean wa Izmir kuelekea mji wa Agri ulioko upande wa mashariki mwa Uturuki.

Video za TRT zinaonyesha timu ya uokoaji ikifika katika eneo la ajali huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa bado hakijafahamika.