Watu 10 wajeruhiwa katika mashambulizi kusini mwa Syria
1 Mei 2020Zaidi ya watu kumi wamejeruhiwa nchini Syria baada ya mashambulizi kwenye ghala la silaha za jeshi katika jimbo la Homs lilioko katikati mwa nchi hiyo, wizara ya ulinzi ya Syria imetanganza. Mashambulizi hayo yanadaiwa kutekezwa na Israel ikilenga kundi la Hezbollah na vikosi vya Rais Bashar Assad.
Televisheni ya taifa nchini Syria mapema imetanganza kutofahamu sababu ya mashambulizi hayo, lakini shirika la kutetea haki za binadamu la Syria lenye makao yake Uingereza limesema mashambulizi hayo yalifanywa na Israel ikitumia makombora kulilenga ghala la zana za kijeshi la kundi la Hezbollah katika kambi ya Ibn a-Haitham.
Mkuu wa shirika hilo, Rami Abdel-Rahman, ameviambia vyombo vya habari vya Syria kuwa zaidi ya raia 10 wa kawaida wamekimbizwa hospitalini baada ya kujeruhiwa katika mashambulizi hayo.
Gavana wa jimbo la Homs, Talal Barazi, pia amesema sababu ya mashambulizi hayo bado haijulikani, ingawa amekiri kuwa ghala hilo linahifadhi silaha za jeshi, bila kueleza iwapo linamilikiwa na kundi la Hezbollah au la.
Mashambulizi hayo ya leo Ijumaa yametokea katika jimbo la Homs, kati kati mwa Syria ambako pia kunapatikana vituo vya jeshi la taifa hilo.
Mashambulizi yalilenga ghala la silaha za jeshi
Hata hivyo, Israel haijatoa tamko lolote kuhusiana na mashambulizi hayo. Israel imekuwa ikifanya mashambulizi ya mara kwa mara, la hivi karibuni likitokea Jumatatu kuyalenga maeneo ya makundi yenye mafungamano na Iran nchini Syria, huku ikisema kamwe haitoikubali Iran kuwa na ushawishi katika mataifa yanaopakana na Israel.
Mnamo Alhamisi Aprili 30.04.2020 shirika la habari la Syria liliripoti kuwa mashambulizi ya helikopta za Israel kutokea eneo la milima ya Golan yalisabadbisha uhabirifu mkubwa wa vifaa vya Syria.
Inafahamika kuwa ghala hilo lilikuwa na zana za kijeshi linamilikiwa na kundi la Hezbollah linaoungwa mkono na Iran, ambalo pia limekuwa likivisaidia vikosi vya Syria katika vita vya miaka tisa.
Katika miezi za hivi karibuni, maafisa wa Israel wameelezea wasi wasi wao kwamba kundi la Hezbollah liko katika harakati za kuanzisha utengenezaji wa makombora nchini Syria.
Hata hiyvo serikali ya Syria imekanusha madai hayo, na kukana kwamba haina maghala yoyote ya makundi yenye mfungamano na Iran.
Vyanzo: APE/DPAE