Watoa uamuzi wa mahakama kuanza kujadili kesi ya Trump
29 Mei 2024Mwendesha mashitaka Joshua Steinglass amewaambia watoa uamuzi, kuwa Trump alishiriki katika njama ya kuwalaghai wapiga kura katika mwaka wa 2016.
Kesi hiyo ya kihistoria, inahusu madai kuwa Trump na washirika wake walikula njama ya kuficha habari za kuwaaibisha wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka wa 2016 kwa kuwalipa watu akiwemo mcheza filamu za ngono aliyedai kuwa yeye na Trump walifanya mapenzi muongo mmoja uliotangulia.
Naye wakili wa Trump Todd Blanche alisema hakuna yeyote kati ya mchezafilamu huyo, Stormy Daniels wala mwanasheria wa Trump aliyemlipa mwanamke huyo, Michael Cohen, anayeweza kuaminiwa.
Soma pia: Trump apandishwa kizimbani kujibu kesi ya jinai
Amesema rais Trump hana hatia, kwa sababu hakufanya uhalifu wowote, na mwendesha mashitaka hakuweza kuthibitisha kikamilifu mashitaka hayo. Ikiwa ni chini ya miezi sita kabla ya uchaguzi ambao Trump anatafuta kurejea katika Ikulu ya White House, umuhimu wa hukumu ya kesi hiyo ni mkubwa kwa Trump mwenye umri wa miaka 77 na kwa Marekani.