Wakati kukiwepo malalamiko ya wananchi kutofaidi rasilimali za taifa hususani wanyamapori, jambo linalochochea kuwepo kwa uwindaji haramu, watanzania sasa wataanza kunufaika na kitoweo cha wanyamapori bila kificho.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo meneja wa Lengo la mradi huo Mwakilishi wa mamlaka ya wanyamapori Tanzania ambaye pia ni meneja wa porii la akiba Rukwa Bw. Goodluck Baragaye amebainisha kuwa lengo ni kudhibiti ujangiri pamoja na kuhamasisha jamii kushiriki uhifadhi.
Hata hivyo kumekuwepo mashaka ya uendelevu wa biashara hiyo, kutokana na hofu hiyo Mkuu wa mkoa wa Katavi Bw. Juma Homera amesema kutokana na idadi ya Wanyama waliopo sambamba na ukubwa wa misitu ya hifadhi, maduka hayo ya nyama yatakuwa endelevu.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kanzisha huduma ya uuzaji wa kitoweo cha wanyamapori, licha ya kwamba zilikuwa zikiuzwa katika hoteli kubwa jijini Dar es salaam na Arusha ambapo wananchi wa kawaida hawakuwa na fursa ya kununua.