AfyaUganda
Wataalamu wasema mripuko wa Ebola nchini Uganda unadhibitiwa
5 Januari 2023Matangazo
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa barani Africa Ahmed Ogwell Ouma, amesema iwapo hakutakuwa na kisa kipya kilizchoripotiwa nchini Uganda kufikia Januari 10 basi mlipuko huo utakuwa umekwisha.
Ouma aliwaambia wanahabari kuwa kufikia sasa kumekuwa na vifo 142 vya Ebola vilivyothibitishwa na vifo 55 katika mlipuko wa Uganda. Majaribio ya chanjo dhidi ya aina ya Ebola ya Sudan yalikuwa yakiendelea.
Aliisifu serikali ya Uganda kwa kuchukua hatua za kuzuia kusambaa kwa Ebola, akisema ilichukua takriban siku 70 za kudhibiti maambukizo hayo huku kukiwa na wagonjwa 142 wakati watu 55 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
Ouma ameeleza kuwa, majaribio ya aina ya kirusi cha Ebola kwa jina Sudan, yanaendelea.