1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Wataalamu waonya juu ya maporomoko ya ardhi Papua New Guinea

7 Juni 2024

Wataalamu wa jiolojia kutoka New Zealand wameoonya kwamba kuna hatari ya kutokea maporomoko mengine zaidi ya ardhi nchini Papua New Guinea katika eneo la kijijini ambako sehemu ya mlima uliporomoka.

https://p.dw.com/p/4gmXS
Papua New Guinea | Eneo la mkasa wa maporomoko ya ardhi
Wakaazi wa kijiji cha Mulitaka Papua New Guinea wakiwa wamekusanyika katika moja ya eneo ambalo limekumbwa na maporomoko ya ardhi.Picha: STR/AFP/Getty Images

Onyo hilo limetolewa leo Ijumaa wakati mamlaka za Papua New Guinea zimesitisha shughuli ya uokozi.

Bado haijafahamika ni watu wangapi waliokufa katika maporomoko ya ardhi yaliyotokea Mei 24, ingawa serikali iliripoti zaidi ya watu 2000 wamezikwa wakiwa hai kwenye janga hilo. 

Soma pia:Juhudi za uokoaji zasitishwa eneo la maporomoko ya ardhi, Papua New Guinea

Umoja wa Mataifa umekadiria kwamba idadi ya waliokuwa ni takriban watu 670.Mpaka sasa ni maiti 11 zilizopatikana kutokana na maporomoko hayo mabaya ya ardhi.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW