Wataalamu wa UN wasema kundi la IS lazidi kujiimarisha Mali
26 Agosti 2023Wapinzani wa kundi hilo wanaofungamanishwa na kundi la kigaidi la Al Qaida wametumia nafasi iliyoachwa wazi kujiimarisha, kufuatia kile kinachoonekana kuwa udhaifu wa makundi yaliyojihami yaliyotia saini mkataba wa amani wa mwaka 2015.
Wataalamu hao wamesema mkwamo wa utekelezwaji wa makubaliano ya amani hasa katika masuala ya upokonywaji wa silaha, uhamasishaji na ujumuishwaji wa watu hao katika jamii, umelipa nguvu kundi hilo la Jama'a Nusrat ul-Islam wa al-Muslimin linalojulikana kama JNIM kupigania uwongozi Kaskazini mwa Mali.
Wataalamu hao wamesema, mashambulizi na vurugu hasa zinazosababishwa na wapiganaji wa IS katika eneo la sahara pia zimefanya mkataba huo wa amani kuwa dhaifu na usioaminika na maafisa wa usalama waliotarajiwa kulinda jamii zinazoshambuliwa.