Wasyria washiriki uchaguzi unaotazamiwa kumpa Assad ushindi
26 Mei 2021Uchaguzi huo wa rais ni wa pili kufanyika tangu mzozo wa vita nchini humo ulipoanza miaka 10 iliyopita na umepuuziliwa mbali na upinzani na nchi za Magharibi, ikiwemo Marekani.
Wadhifa huo wa urais umeshikiliwa na jamaa wa familia ya Assad kwa miongo mitano.
Soma zaidi: Wafuasi wa rais Assad washambuliwa Lebanon
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amesema nchi yake inaungana na Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uingereza katika kuhimiza kukataliwa kwa jitihada za utawala wa Assad kurejesha uhalali bila kuheshimu haki za binaadamu na uhuru wa watu wa Syria.
Akizungumza baada ya kupiga kura yake katika kitongoji cha Douma nje ya mji mkuu Damascus, Assad alizishambulia nchi ambazo zimeupuzia uchaguzi huo kutokuwa halali, akisema mengi ya mataifa hayo yana historia ya ukoloni na kuwa Syria kama taifa haijalishwi na kauli za aina hiyo.