1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washirika wa Ukraine wajadili namna ya kuipa silaha zaidi

15 Februari 2023

Washirika wa Magharibi wanaoiunga mkono Ukraine wanakutana kwa siku ya pili kwa lengo la kuharakisha uwasilishwaji wa zana za kivita kwa Kyiv, ambayo pia inaomba ndege za kivita.

https://p.dw.com/p/4NUzw
Belgien Brüssel | EU-Gipfel | Rede Wolodymyr Selenskyj im EU-Parlament
Picha: Kenzo Tribouillard/AFP

Baada ya kupata ahadi ya kupewa vifaru, mifumo ya ulinzi wa mashambulizi ya kutokea angani na makombora, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesisitiza kuhusu ombi lake la ndge za kivita kutoka kwa nchi za Magharibi.

Urusi:NATO inazidi kujiingiza katika mzozo wa Ukraine

Lakini washirika wanaokutana katika makao makuu ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO mjini Brussels wanaangazia zaidi hoja ya kuhakikisha kuwa wanajeshi wake wanapata silaha, magari ya kivita na mifumo ya ulinzi wanayohitaji katika uwanja wa mapambano ili kuyadhibiti mashambulizi mapya ya Urusi.