SiasaAsia
Washirika wa Imran Khan waongoza uchaguzi Pakistan
9 Februari 2024Matangazo
Khan alizuiwa kushiriki uchaguzi wa Alhamis (Februari 8) na chama chake cha Pakistan Tahreek-e-Insaf ( PTI) kilizuwiwa kufanya mikutano ya kampeni na kuondolewa kwenye karatasi za kura, na hivyo kuwalazimu wanachama wake kushiriki kama wagombea huru.
Soma zaidi: Mahakama ya Uchaguzi Pakistan yaamuru kuharakishwa matokeo
Lakini matokeo ya awali yanaonesha wafuasi wa PTI mpaka sasa wameshinda karibu vita 49 katika bunge la taifa lenye jumla ya vitia 266, dhidi ya viti 42 vya chama cha Pakistan Muslim League- Nawaz (PML-N) na kile cha Pakistan Peoples Party (PPP) baada ya zaidi ya nusu ya majimbo kukamilisha hesabu.