1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washambuliaji wawili wauwawa na polisi mjini Istanbul

6 Februari 2024

Polisi wa Uturuki wamewapiga risasi na kuwaua washambuliaji wawili wa shirika la kuegemea siasa za mrengo wa kushoto na ambalo limetajwa kuwa la kigaidi na mamlaka nchini humo.

https://p.dw.com/p/4c6Ti
Eneo la mkasa mjini Istanbul
Eneo la mkasa mjini Istanbul Picha: Francisco Seco/AP/picture alliance

Maafisa wamesema watu hao, mwanamume na mwanamke, walishambulia kituo cha ukaguzi wa usalama nje ya mahakama kuu mjini Istanbul, na kumuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine watano.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya amesema washambuliaji hao walikuwa wanachama wa Chama cha Ukombozi wa watu DHKP-C, kundi la kuegemea siasa za mrengo wa kushoto ambalo limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Uturuki tangu miaka ya 80.

Kundi hilo, hata hivyo halijatoa taarifa yoyote kudai kuhusika na shambulio la leo.

Rais Recep Tayyip Erdogan amevipongeza vikosi vyake vya usalama kwa kuwakabili washambuliaji hao.

Kundi hilo ambalo linachukuliwa kuwa la kigaidi na Marekani, limekuwa likipambana dhidi ya ushawishi wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati na duniani kote.