Waromania wanashiriki uchaguzi wa bunge
1 Desemba 2024Matangazo
Uchaguzi huu unafanyika wiki moja baada ya kumalizika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, uliompa ushindi mgombea wa siasa kali za mrengo wa kulia Calin Georgescu. Uchaguzi huo umeitumbukiza nchi hiyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya naNATO katika mvutano kutokana na madai ya ukiukwaji wa sheria za uchaguzi pamoja na uingiliaji wa Urusi. Uchaguzi wa bunge leo hii utachagua serikali mpya na waziri mkuu na kuamuwa sura ya bunge jipya la viti 466. Uchaguzi wa rais wa duru ya pili umepangwa kufanyika tarehe 8 Desemba ambapo Georgescu atapambana na mwanamageuzi Elena Lasconi wa chama cha USR.