1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Wapiganaji wa Tigray wakabidhi silaha

11 Januari 2023

Msemaji wa vikosi vya wapiganaji wa Tigray Getachew Reda anasema wamekabidhi silaha nzito kama sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa na serikali ya Ethiopia mwishoni mwa mwaka uliopita kuumaliza mzozo wa miaka miwili.

https://p.dw.com/p/4M0Zb
Äthiopien | Kämpfer der Tigray People's Liberation Front
Picha: Ben Curtis/AP Photo/picture alliance

Reda ameandika mapema leo Jumatano katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twita kwamba timu ya waangalizi wa Umoja wa Afrika wamethibitisha makabidhiano hayo ya silaha.

Ameleezea matumaini kwamba hatua hiyo itasaidia kwa kiwango kikubwa utekelezaji kamili wa mkataba wa amani.

Wapiganaji wa Tigray wanataka vikosi vya wanajeshi kutoka nchi jirani ya Eritrea ambao wamekuwa wakipigana upande wa Ethiopia, na ambao hawakuwa sehemu ya mchakato wa amani, waondoke. Inaripotiwa wapiganaji hao kutoka Eritrea bado wako katika baadhi ya jamii za Tigray.