1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina wavamia mipaka ya Israel

16 Mei 2011

Wapalestina kadhaa wameuawa na mamia wengine wamejeruhiwa katika ghasia mpya zilizotokea hiyo jana yaani siku ambayo Wapalestina wanaiita "Siku ya Nakba" yaani siku ya maafa.

https://p.dw.com/p/RO5j
Palestinians carry Palestinian flags as they arrive near the Lebanese-Israeli border during a rally marking "nakba," or "catastrophe," the term used by Palestinians to describe the uprooting they suffered at the time of Israel's founding on May 15, 1948, in the southern border village of Maroun el-Rass, Lebanon, Sunday, May 15, 2011. Two Lebanese security officials say four people in Lebanon were killed when Israeli soldiers opened fire at protesters who approached the border with Israel. The Arabic writing reads:" Iran's garden." (Foto:Mohammed Zaatari/AP/dapd)
Wandamanaji wa Kipalestina wakiadhimisha "Siku ya Nakba"Picha: dapd

Siku hiyo, Wapalestina wanaomboleza kupoteza makaazi yao miaka 63 iliyopita, kufuatia kuundwa kwa taifa la Israel. Ghasia za hiyo jana zilizuka, baada ya maelfu ya wakimbizi wa Kipalestina kutoka Syria kuivamia mipaka ya Israel.

Kwa mara ya kwanza baada ya miongo kadhaa, hiyo jana maelfu ya watu kutoka Syria waliuvamia mpaka unaotenganisha nchi hiyo na Milima ya Golan inayokaliwa na Israel. Vikosi vya Israel vilijibu kwa kuwafyatulia risasi raia hao. Ripoti zinasema watu 12 wameuawa na mamia wengine wamejeruhiwa. Kwa mujibu wa ripoti za mashahidi, zaidi ya watu 20 walifanikiwa kujipenyeza katika kijiji cha mpakani Mashd el Shams, ambako polisi wa Syria walishindwa kuwazuia waandamanaji hao kuvuka mpaka.

Hii ni mara ya kwanza tangu vita vya Mashariki ya Kati vya 1973, kwa kitendo kama hicho kutokea katika mpaka huo wa Syria na Israel, unaolindwa vikali. Msemaji wa jeshi la Israel Avital Leibovich anawalaumu maafisa wa Syria kwa machafuko yaliyofikia kiwango hicho.Amesema:

"Serikali ya Syria makusudi inajaribu kuufanya ulimwengu utazame kwengiko badala ya matumizi ya nguvu dhidi ya raia wake wenyewe."

Wapalestina waadhimisha "Siku ya Nakba"

Palästina Israel Konflikt Nakbah
Vijana wa Kipalestina wakirusha mawePicha: picture-alliance/dpa

Maandamano yalifanyika hata katika Ukanda wa Gaza ambako hadi watu 70 walijeruhiwa baada ya waandamanaji wa Kipalestina kuvuka vizuizi vilivyowekwa na Hamas na kusonga mbele hadi kwenye kituo cha ukaguzi cha Israel,Eres. Na kwenye kituo cha mpakani cha Kalandia huko Ramallah,waandamanaji wa Kipalestina waliwarushia mawe wanajeshi. Katika mji huo wa Ramallah, siku ya Nakba iliadhimishwa kwa maandamano ya maelfu ya watu waliokusanyika kwenye uwanja wa Manara. Vingora vililia kuwakumbuka wakimbizi wa Kipalestina.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipohotubia kikao cha wiki cha baraza la mawaziri wake alisema kuwa anasikitika kuwa wafuasi wa itikadi kali wameibadili siku ya uhuru wa Israel kuwa siku ya vurugu.

Mwandishi: Bamu,Andreas/ZPZ/P.Martin

Mhariri: Abdul-Rahman