1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Wanyarwanda wakumbuka miaka 30 ya mauaji ya kimbari

7 Aprili 2024

Rwanda leo Jumapili 07.04.2024 imetimiza miaka 30 tangu yafanyike mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya walio wachache ya Watutsi. Wahutu walio waliowasaidia Watutsi pia waliuawa manmo mwaka 1994.

https://p.dw.com/p/4eVtD
Reclaiming History - Völkermord in Ruanda 1994
Picha: Ben Curtis/AP Photo/picture alliance

Rais wa Rwanda Paul Kagame amewasha mwenge hii ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji hayo katika eneo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari katika mji wa Kigali. Mauaji hayo yalitokea Aprili 7 mwaka 1994 ambapo zaidi ya wahanga 250,000 wanaaminika walizikwa katika eneo hilo.

Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994
Katikati ya wanajeshi ni Rais wa Rwanda Paul Kagame katika siku ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya kimbari tarehe 07.04.2000Picha: Marco Longari/dpa/picture alliance

Bendi ya jeshi ilipiga nyimbo za huzuni, wakati rais Kagame alipoweka mashada ya maua kwenye makaburi ya halaiki, akiwa amezungukwa na viongozi wa kigeni wakiwemo wakuu kadhaa wa nchi za Afrika na  aliyekuwa rais wa Marekani wakati wa mauaji hayo Bill Clinton.

Soma Pia: Paul Kagame: Shujaa au Dikteta?

Clinton, amesema kushindwa kuepusha mauji hayo ya halaiki nchini Rwanda ni kosa kubwa lililofanywa na utawala wake.

Nia ya kuzuia mashambulizi ya kimbari Rwanda

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macro katika ujumbe wake siku ya leo amesema Ufaransa na washirika wake wa Magharibi na wa Afrika wangeliweza kuyazuwia mauaji hayo lakini hawakuwa na nia ya kufanya hivyo.

Mwanadiplomasia wa zamani wa jamhuri ya Czech, Karel Kovanda, aliyekuwa balozi wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kutamka hadharani matukio ya mwaka 1994 kuwa ni mauaji ya halaiki, karibu mwezi mmoja baada ya mauaji hayo kuanza, amesema mauaji hayo si jambo la kusahaulika.

Wahanga wakumbuka mauaji ya kimbari ya mwaka 1994
Chantal Uwanyirigira ni miongoni mwa watu walionusurika kifo katika mauaji ya kimbari ya mwa 1994 nchini Rwanda. Alikimbilia kanisani na familia yake ili kujinusuru. Picha: DW

Kumbukumbu hiyo ya Rwanda inakumbushia kipindi cha kutisha katika taifa hilo la Afrika Mashariki ambapo jamii ya Wahutu wenye msimamo mkali walifanya mauaji ya halaiki yaliyosabisha umwagikaji damu nchini Rwanda. Mauaji hayo ni mabaya zaidi kuwahi kutokea katika ya karne ya 20. Majirani walishambuliana kufikia hatua ya kuisambaratisha nchi yao.

Soma Pia: UN yaitaka Uingereza kuachana na mpango wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda

Umoja wa Mataifa umesema karibu watu 800,000 waliuawa nchini Rwanda. Hadi leo hii, makaburi ya halaiki yanaendelea kugundulika katika nchi hiyo yenye watu karibu milioni 14. 

Mauaji ya Rais wa Juvenal Habyarimana

Mauaji ya Rais wa Juvenal Habyarimana wa kabila la Hutu mnamo usiku wa Aprili 6, baada ya ndege yake kudunguliwa katika anga ya Rwanda, yalichochea Wahutu wenye msimamo mkali na wanamgambo wa "Interahamwe" kufanya mashambulizi. 

Wahanga waliuliwa kwa kuwapiga risasi, kupigwa vibaya na wengine walichinjwa.
Mauaji yaliyochochewa na propaganda za kuwapinga Watutsi zilizotangazwa kwenye Televisheni na redio. Wanawake- wapatao 250,000 walibakwa, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Soma Pia: Macron asema Ufaransa ingeweza kusitisha mauaji Rwanda

Mnamo mwaka 2002, Rwanda ilianzisha mahakama za jumuiya ambapo wahanga walisikiliza watu waliowatendea maovu ingawa watetezi wa haki wamesema haki zilikiukwa kwenye mahakama hizo.

Kwa sasa, vitambulisho vya Rwanda haviandikwi kama mtu ni Mhutu au Mtutsi.
Wanafunzi wa shule za upili hujifunza kuhusu mauaji ya halaiki kama sehemu ya mtaala unaodhibitiwa vilivyo.

Nyumba za makumbusho Rwanda

Rwanda ina nyumba za makumbusho zaidi ya 200 za mauaji ya kimbari, mnamo mwaka jana 2023, nyumba nne kati ya hizo ziliwekwa kwenye orodha ya Turathi za Dunia ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamnaduni, (UNESCO).

Mafuvu ya vichwa ya wahanga wa mauaji ya kimbari kwenye nyumba ya makumbusho nchini Rwanda
Mafuvu ya vichwa ya wahanga wa mauaji ya kimbari kwenye nyumba ya makumbusho nchini RwandaPicha: SIMON MAINA/AFP

Kwenye nyumba hizo za makumbusho yapo mafuvu ya vichwa, vipande vya mifupa, nguo zilizochanika na picha za maiti zilizorundikana pamoja na bunduki, mapanga na silaha nyingine zilizotumika kutekeleza mauaji hayo ya Kimbari yaliyotokea tarehe 7, Aprili mwaka 1994.

Chanzo: AFP