1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake 1000 kwa tuzo ya Nobel

Joachim Schubert-Ankenbauer / Maja Dreyer6 Oktoba 2005

Ingawa katika miaka miwili iliyopita wanawake wawili wamepata tuzo ya Nobel, mmojawapo ni Wangari Maathai kutoka Kenya, bado idadi ya wanawake walioshinda kupata tuzo za Nobel ni ndogo sana. Kwa miaka kadhaa sasa shirika moja kutoka Uswisi linalowakilishi wanawake wote wanajitolea kuleta amani, linalenga kubadilisha hali hii.

https://p.dw.com/p/CHed
Wangari Maathai alipokabidhiwa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2004
Wangari Maathai alipokabidhiwa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2004Picha: AP

„Wanawake 1000 wapate tuzo ya amani ya Nobel“ – hili ni jina la shirika lililoanzishwa na Mswisi, Ruth-Gaby Vermot-Mangold. Bibi huyu ambaye ana umri wa miaka 64 ni mjumbe wa bunge la Uswisi na vile vile wa bunge la Umoja wa Ulaya. Kazi yake ya kusaidia wakimbizi na kuimarisha haki za bindamu barani Ulaya ilimsaidia kupata wazo la kuanzisha shirika lake. Anaeleza:

„Wakati huo nilikuwa spika wa mambo ya nchi za Balkan, kwa hivyo nilipasafiri mara nyingi. Niliwatembea wanawake katika makambi ya wakimbizi na niliona kwamba kwa jumla ni wanaume waliokata tamaa. Wanawake walijipa moyo na ndiyo ni wale walioleta maendeleo muhimu zaidi. Hawajaangalia tu hali yao ya usalama, lakini walitaka kuendelea na maisha yao. Walisema: Tufanye nini ili kuendelea kuishi?“

Halafu Bibi Vermot-Mangold alianzisha shirika dogo lililoenea duniani kote. Leo kuna mtandao wa wanawake kutoka kila pembe ya dunia. Lengo lao ni: badala ya mwanamume, wanawake 1000 wapewe tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu.

Idadi hiyo ya 1000 ilisababisha maswali na mashaka mengi. Kwa mfano: kweli ni lazima iwe wanawake 1000 kusawazisha kazi na mwanamume mmoja? Bibi Vermot-Mangold anajibu bila wasiwasi:

„Idadi hii ni ishara tu. Tunataka kubadilisha sifa ya wanawake duniani kote. Wote wanawaheshimu wale wanaume kadhaa waliopata tuzo ya Nobel kama mfalme wa amani ingawa hawafanyi kazi katika daraja la chini. Nataka dunia kote iangalie wanawake wale 1000, katika vijiji vyao, ambapo wanaleta amani kwa watu wa kawaida.“

Kulingana na shirika la Bibi Vermot-Mangold, kuleta amani haimaanisha tu kuzuia vita, lakini kuleta elimu, afya, maji safi, kupambana na ubaguzi, hofu na vurugu. Kwa hiyo wanawake 1000 walichaguliwa kutoka mashirika mbali mbali ya nchi 150 wanaoleta amani kwa njia hiyo. Lakini kwa wanawake wachache hawana nafasi tena kupendekezwa kwa tuzo hiyo. Mmojawapo ni msichana wa umri wa 14 kutoka sehemu ya Tshetshenia, eneo la vita nchini Urusi. Msichana huyu aliwakusanya watoto kila asubuhi kuwafundisha na akawaambia: Angalia, ikiwa wakati amani itakapofika nchini Tsheshenia watoto huwa ni wapumbavu, wataanza tena vita. Msichana huyu lakini aliuawa, amefariki dunia.

Mpaka sasa shirika la „wanawake 1000 kwa tuzo ya amani ya Nobel“ limeshaleta mafanikio makubwa kwa kuunda mtandao wa wanawake duniani. Lakini hii haitoshi, anasema Bibi Vermot-Mangold: “Tumesema tu kwa nguvu na bila kukata tamaa: tunataka tuzo hiyo ili wanawake wathaminiwe.“