1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Washirika wa Imran Khan washinda vita vya bunge Pakistan

11 Februari 2024

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi nchini Pakistan yametangazwa hii leo huku wagombea binafsi walioungwa mkono na waziri mkuu wa zamani aliye gerezani, Imran Khan, wakishinda vita 101 kati ya 264 vya bunge la taifa

https://p.dw.com/p/4cGhT
Wafanyakazi wa tume ya uchaguzi nchini Pakistan wahesabu kura baada ya kukamilika kwa zoezi la kupiga kura mnamo  Februari 8, 2024
Wafanyakazi wa tume ya uchaguzi nchini Pakistan wahesabu kuraPicha: PPI/Zuma/picture alliance

Takwimu hizo zimechapishwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo saa 60 tangu kufanyika uchaguzi huo mnamo siku ya alhamisi.

Hii ni mara ya kwanza kwa matokeo ya uchaguzi wa Pakistan kuchelewa kutangazwa na hali hiyo imezusha maswali kuhusiana na uhalali wake.

Chama cha Khan kilitangaza mgomo wa kitaifa

Chama cha Khan tayari kilitangaza  kuwa kitaitisha mgomo wa taifa zima iwapo tume isingemaliza kutangaza matokeo hayo leo jumapili.

Soma pia: Mahakama ya Uchaguzi Pakistan yaamuru kuharakishwa matokeo

Chama cha waziri mkuu mwingine wa zamani Nawaz Sharif kimepata viti 75 na kukifanya kuwa ndiyo kikubwa zaidi bungeni.

Mwanasiasa huyo amesema chama chake tayari kinafanya mazungumzo na makundi mengine ili kuunda serikali ya mseto baada ya kushindwa kupata wingi wa viti kwenye bunge la taifa.