WANAMGAMBO WAFANYA FUJO-LIBERIA:
10 Desemba 2003Matangazo
MONROVIA: Nchini Liberia wanamgambo waliovunjika moyo wamefanya ghasia baada ya kugundua kuwa hawatolipwa moja kwa moja,zile Dola 300 walizoahidiwa kupewa kama sehemu ya mpango wa kutoa silaha zao.Siku ya jumanne Umoja wa Mataifa ulisema wapiganaji hao watapewa Dola 75 pale watakapokabidhi silaha zao,ikiwa ni pamoja na chakula na msaada wa kujijumuisha tena na jamii.Na wakaarifiwa kuwa sehemu nyingine ya pesa itatolewa baada ya kukamilishwa mpango wa kukusanya silaha na wapiganaji hao kujijumuisha na jamii zao.Kwa upande mwingine Umoja wa Mataifa umetoa ratiba mpya inayohusika na ukusanyaji wa silaha na kusaidia kiasi ya wapiganaji 40,000 kuanza maisha ya kawaida.