1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tisa wauawa kijiji kinachodhibitiwa na majeshi ya EAC Kongo

7 Agosti 2023

Watu tisa wameuawa katika kijiji kinachodhibitiwa na vikosi vya kijeshi vilivyotumwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ili kudhibiti ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4UqbN
Demokratische Republik Kongo | Soldaten nach Kämpfen mit Rebellengruppe M23
Picha: Guerchom Ndebo/AFP/Getty Images

Wakazi wa kijiji cha Marangara katika eneo la Rutshuru katika jimbo la Kivu Kaskazini walishambuliwa na watu wenye silaha usiku wa kuamkia Jumapili.

Kiongozi mmoja wa eneo hilo, ambaye aliomba kutotajwa jina kutokana na sababu za kiusalama, amesema nyumba tano pia zilichomwa moto na kwamba wahusika bado hawajafahamika.

Soma zaidi: Mapigano yazuka tena Rutshuru kati ya M23 na Mai Mai

Lakini kiongozi mwengine wa mashirika ya kiraia, ambaye pia hakutaka jina lake litajwe, amesema washambuliaji walikuwa waasi wa M23 wanaotuhumiwa kwa ukatili dhidi ya raia katika eneo hilo.