Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waendelea kuondoka Mali
22 Oktoba 2023Matangazo
Kuondoka siku ya Jumamosi (Oktoba 21) kwa Kikosi hicho cha amani cha Umoja wa Mataifa kinachofahamika kama MINUSMA, kumeongeza hofu ya kuongezeka kwa mapigano kati ya wanajeshi wa Mali na makundi ya wanamgambo wanaotaka kulidhibiti eneo hilo.
Soma zaidi: Walinda amani wa umoja wa Mataifa waondoka Mali
Taarifa ya kuondoka kwa wanajeshi hao ilithibitishwa na jeshi la Chad ndani ya kikosi hicho.
Kuondoka kwa wanajeshi 11,600 na maafisa wa polisi 1,500 wa MINUSMA kunatarajiwa kukamilika Desemba 31.